.
17th October, 2016
Mwili wa mwanafunzi wa darasa la nane wa shule ya msingi ya Subukia kaunti Nakuru umehifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Nyahururu baada ya kufariki kupitia madai ya kuchapwa na kujeruhiwa kichwani na mwalimu. Kwa mujibu wa idara ya elimu kaunti ndogo ya Subukia, uchunguzi umeanzishwa kubaini ukweli wa madai hayo.