.
15th January, 2022
Kinara wa ODM Raila Odinga amekashifu naibu rais William Ruto akisema kuwa ameshindwa kutekeleza kazi na hivyo sasa ampe nafasi Odinga kuhudumia wakenya. Odinga ambaye amefanya mkutano wa kisiasa eneo la thika kaunti ya Kiambu amesema kuwa kwa miaka tisa Ruto amekuwa serikalini hakuna alilo nalo kuonyesha na hivyo ni wakati kuondoka serikalini.