.
25th October, 2021
Naibu rais William Ruto amewatahadharisha wakenya dhidi ya kuhadaiwa na ahadi ambazo amedai ni za uongo na wanasiasa wanaotafuta uongozi. Akizungumza katika mikutano ya hadhara katika eneo la kibwezi kaunti ya Makueni, Ruto amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo haziwezi kutimizwa.