22nd June, 2021
Siku chache kabla ya muungano wa walimu nchini Knut kuandaa kongamano la wajumbe watakaoshiriki katika uchaguzi wa viongozi wapya, mvutano bado ungalipo kuhusu mbinu itakayotumika katika uchaguzi huo. Baada ya katibu mkuu Wilson Sossion kupendekeza kuwa uchaguzi huo uandaliwe kwa njia ya mtandao, leo kundi linalompinga limependekeza kwamba uchaguzi huo uandaliwe kwa njia itakayomruhusu kila mjumbe kushiriki moja kwa moja na kwa kuzingatia kanuni za kuzuia maambukizi ya corona. Wamesema wizara ya afya imewapa kibali cha kuandaa uchaguzi huo katika uga wa michezo wa Ruaraka tarehe 26 mwezi huu