×
× KTN NEWS News Business Sports Politics Features Live Schedule E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Baba awadunga kisu wanawe wawili katika eneo la Nyandarua, watoto hao wako mahututi hospitalini

20th June, 2021

Watoto wawili wamelazwa wakiwa mahututi katika hospitali moja mjini Nyahururu baada ya kudungwa kisu na baba yao kufuatia mzozo wa nyumbani katika mtaa wa ziwani ulioko kaunti ya Nyandarua. Ken Mburu anasemekana kupandwa na mori na kuwadunga kisu watoto hao, kuitia moto nyumba yake kabla ya kujaribu kujitoa uhai kwa kujidunga kisu jana jioni.  Alimdunga kisu mara kumi mgongoni mwanaye msichana wa umri wa miaka saba huku msichana mdogo wa umri wa mwaka mmoja akimdunga kisu mara tano Mgongoni. Baba huyo aliyejidunga kisu tumboni pamoja na wanawe wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Nyahururu huku jiraniye Mburu akisema kuna uwezekano hatua ya Mburu ilitokana na ugomvi na mkewe ambaye hakuwa nyumbani wakati wa tukio.

.
RELATED VIDEOS