16th June, 2021
Polisi Ruiru katika kaunti ya Kiambu wanamtafuta mwanamume mmoja anayeshukiwa kumdunga kwa kisu na kumwua mkewe wa miaka 29. Inakisiwa kuwa Rosemary Waceke alidungwa kisu usiku wa kuamkia leo katika nyumba yao iliyoko katika mtaa wa ruiru wataalam. Rafiki wa mwendazake aliambia waandishi wa habari kuwa ndoa yao ilikumbwa na ugomvi wa mara kwa mara. Sasa familia ya Waceke ambaye mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha City mjini Nairobi wanataka haki kwani mshukiwa hajashikwa na polisi.