29th May, 2021
Huenda sherehe za sikukuu ya Madaraka zikakosa kuandaliwa katika uwanja uliokarabatiwa wa Jomo Kenyatta mjini Kisumu na kufanyika katika ikulu ndogo ya Kisumu. Hatua hio imetokana na tahadhari zilizoko za kuzuia kuenea kwa virusi vya korona wakati maambukizi mapya yakinakiliwa sehemu hiyo. Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuingia Kisumu hapo kesho.