.
12th May, 2021
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu watakuwa wakisherehekea siku kuu ya idd ul fitre hiyo kesho japo kuna wale wanaotarajiwa kusherehekea siku ya ijumaa kulingana na tarehe walioanza mfungo wa Ramadhan. Katika jiji la Mombasa imekuwa shamrashamra ya kipindi cha lala salama ambapo maduka ya nyama na bidhaa nyingine yalifurika wanunuzi japo bado kunao wauzaji walioambulia patupu.