Chama cha ANC yadai ODM ina mpango wa kuiba kura katika uchaguzi mdogo wa Matungu
02, Mar 2021
Chama cha ANC kimeripoti leo katika ofisi za iebc madai kuwa chama cha ODM kina njama ya kuiba kura katika uchaguzi mdogo wa matungu ulioratibiwa kufanyika tarehe 4 alhamisi. Chama hicho kinadai kuwa chama cha ODM kilifanya mkutano wa faragha na maafisa wa iebc usiku wa kuamkia jumanne. Iebc ikipokea malalamishi hayo na kusema kuwa imeanzisha uchunguzi.