3rd February, 2021
Waziri wa Elimu Prof George Magoha amemteua Bi Agnes Mercy Wahome kuwa afisa mkuu mtendaji wa bodi ya kuwapa nafasi wanafunzi katika vyuo vikuu na vyuo vya kadri nchini KUCCPS. Bi wahome amekuwa akiishikilia nafasi hio tangu novemba mwaka jana kabla ya kuthibitishiwa leo baada ya aliyekuwa afisa mkuu wa bodi hiyo john muraguri kuchukua likizo ya kustaafu. Bodi hio ni ile ilifahamika zamani kama joint admission board ( JAB ). Wahome alijiunga na bodi hiyo mwaka wa 2018 kama meneja wa utafiti.