x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Huduma Duni Kabarnet: Hospitali ya rufaa ya Baringo imemulikwa kwa madai ya kutoa huduma duni

06, Dec 2020

kwa mara nyingine tena, hospitali ya rufaa ya kaunti ya Baringo iliyoko mjini kabarnet, imemulikwa kwa madai ya kutoa huduma duni kwa wagonjwa swala ambalo limewapa mahangaiko wakaazi wa mji wa kabartnet na viunga vyake. hii ni baada ya kubainika kuwa wakaazi wanaofika hospitalini hapo kutafuta huduma za dharura nyakati za usiku, hawashughulikiwi kwani mara nyingi hakuna mhumu yeyote anayepatikana. Katika picha za simu zilizonaswa na mmoja wa wakaazi wa eneo hilo waliofika katika hospitali hiyo kutafuta hudumu usiku wa kuamkia leo, wagonjwa katika hospitali hiyo wanaonekana wakilazimika kusubiri usiku kucha kabla ya kupata huduma. wengi wanalazimika kulala kwenye madawati usiku kucha. kadhalika hakuna mfumo wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kwani wagonjwa wanaruhusiwa kuingia bila hata kupimwa joto wala kupitia kanuni zozote za afya kuzuia maambukizi. usimamizi wa hospitali hiyo baado haijazungumzia hali hiyo ya kusikitisha.

Feedback