25th November, 2020
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Nick Mwendwa amekanusha kuhusika kwa sakata ya mchuano wa Chan wa mwaka 2018 ambapo zaidi ya shilingi milioni 155 inaripotiwa kufujwa. Akizungumza mbele ya kamati ya bunge inayohusika na akaunti za umma, Mwendwa alisema kuwa hakuhusika katika utoaji wa zabuni kwa kampuni zilizojukumishwa kuandaa viwanja vya humu nchini. Hata hivyo wanachama wa kamati hiyo walitaka kujua ni kwa nini mwendwa alipendekeza mashirika matatu kupewa zabuni na Wizara ya Michezo.