25th November, 2020
Mwanaume mwenye umri wa miaka 63 kutoka kijiji mayungu kata ya mukulusu eneo bunge la shinyalu kaunti ya kakamega anazuiliwa na polisi katika kituo Shisasari baada ya kumpiga mkewe beatrice imbwaka hadi kufariki. Inadaiwa kuwa mshukiwa alianza kumpiga mwendazake mzozo ulipozuka kuhusiana nani mmiliki halisi wa shilingi 600 ambazo mkewe alikua ameuza pombe aina ya chang'aa. Mkewe alipokataa kumpa hela hizo inadaiwa alimpiga kitutu hadi kumuua