.
18th November, 2020
Viongozi wa kidini wakiongozwa na Maaskofu na Masheikh katika eneo la magharibi mwa Kenya wamekongamana mjini Kakamega kujadili kuongezeka kwa kasi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na virusi vya Korona katika kaunti ya Kakamega. Kwa kauli moja wakikubaliana kuwatimua waombolezaji wowote wanaozidi idadi ya mia mbili kwenye maziko, kupinga mikutano ya kisiasa pamoja na kutaka mikutano na siasa za Bbi zahirishwe hadi virusi vya Korona vipungue nchini.