Viongozi wa kidini wapaaza hisia zao, wasisitiza hoja zao ziekwe kwenye ripoti ya BBI
11, Nov 2020
Vuta nikuvute ya kujumuishwa kwa mapendekezo mapya kwenye ripoti ya BBI inaendelea kuibua hisia tofauti miongoni mwa viongozi wa kisiasa na wa kidini. Baadhi ya viongozi na haswa wa mrengo unaounga mkono Rais Uhuru Kenyatta Na Kinara wa Odm Raila Odinga wanasema nafasi ya kuongeza mapendekezo imekuwepo hivyo ni vyema shughuli hio kuendelea kama ilivyoratibiwa. Baadhi ya viongozi wa kanisa wanasema kuwa mapendekezo waliyotoa hayakuzingatiwa.