x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Wafanyakazi wa Tuskys magic, Nakuru wamelemaza shughuli baada ya madai ya kutolipwa mishahara yao

31, Oct 2020

Wafanyakazi katika duka la jumla la tuskys magic mjini Nakuru, hii leo wamelemaza shughuli katika duka hilo. ni baada ya madai kuwa licha ya kutolipwa mishahara yao ya miezi mitatu iliyopita, mwajiri wao sasa amewasimamisha kazi ghafla pasi na fidia. wafanyikazi hao wapatao hamsini wanasema kuwa kitumbua chao kiliingia mchanga tangu mapema mwaka huu, mwanzoni mwa maambukizi ya virusi vya korona.

Feedback