Mjarabu wa KNEC: Gredi 4 na darasa la 8 kuanza mtihani, mjarabu kutathmini utayari wa watoto
21, Oct 2020
Huku mtihani wa majaribio wa wanafunzi wa gredi ya 4 na darasa la 8 ukianza, shule mbili za sekondari katika kaunti ya Mombasa zimefungwa baada ya walimu kumi na watano kupatikana na virusi vya korona. Kulingana na kamishena wa kaunti ya Mombasa, Gilbert Kitiyo, walimu 11 wa shule ya upili ya Tononoka walipatikana na virusi vya korona nayo shule ya Star of the Sea ikipatikana walimu wanne wenye covid?19. Kwa sasa shule hizo zitasalia kufungwa kwa majuma mawili