Wakazi wa Mihang'o waandamana barabarani kushinikiza wapewe hatimiliki ya ardhi
07, Oct 2020
Wakazi wa eneo la Mihango hapa jijini Nairobi wamefanya mandamano ya Amani kuishinikiza serikali kuingilia kati ili kuwasaidia kupata hatimiliki ya vipande vya ardhi walivyonunua zaidi ya miaka 20 iliyopita. Wakaazi hao wanasema wana wasiwasi kwani huenda wakahamishwa kwenye vipande vyao wakati wowote iwapo serikali haitaingilia kati.