x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Familia yaomba usaidizi baada ya mpendwa wao kuzama majini Uganda

02, Dec 2019

Familia moja kutoka kijiji cha Siekunya eneo la Nambale kaunti ya Busia sasa inaiomba serikali kuingilia kati ili kusaidia kuopoa maiti ya mpendwa wao aliyezama baada ya mashua yao kuzama kwenye mto Ashwa wilaya ya Pader nchini Uganda wiki moja iliyopita. Joseph Wafula mwenye umri wa miaka 42 aliyekuwa akifanya kazi kama mtaalamu wa maji alikuwa katika shughuli za kikazi eneo hilo kabla ya mashua  yao kuzama. Mashua hiyo ilikuwa imebeba watu 4 akiwemo marehemu, ila ni wawili pekee walionusurika. Mbunge wa Nambale John Bunyasi amelaumu serikali ya Uganda kwa kujikokota katika shughuli ya kuopoa maiti ya mwendazake

POPULAR NEWS VIDEOS


Feedback