17th August, 2016
Kijiji cha Ndabibit eneo bunge la Kuresoi kusini kaunti ya Nakuru, kinaendelea na sherehe za ushindi wa msichana wao Faith Chepngetich Kipyegon katika mbio za mita 1500 kwenye mashindano ya olimpiki jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Wakaazi hao hatahivyo,wamelalama kwamba kijiji hicho bado hakijaunganishwa na nguvu za umeme kama anavyoarifu Victor Ogalle aliyewatembelea.
Faith Kipyegon anyakua dhahabu Rio
MKENYA Faith Chepng'etich Kipyegon amejishindia nishani ya dhahabu kwenye mbio za mita elfu moja mia tano akina dada, kwenye mashindano ya Olimpiki yanayoendelea jijini Rio, Brazil.
Faith ambaye ameishindia Kenya nishani ya tatu dhahabu kwenye mashindano hayo, amemshinda bingwa wa dunia, Genzebe Dibaba wa Ethiopia kwa kukamilisha mbio hizo kwa muda wa dakika nne sekunde nane.
Ushindi wa Kipyegon unajir