x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Raila Odinga awaongoza viongozi wa upinzani kuwafariji wenyeji wa Huruma

03, May 2016

Viongozi wa upinzani Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula walifika jioni hii katika mtaa wa Huruma hapa Nairobi ili kujiunga na wenyeji waliokumbwa na mkasa wa jumba kuporomoka siku ya Ijumaa iliyopita, ambapo watu 22 kufikia sasa wanaripotiwa kufariki. Msafara wa viongozi hao uliwavutia wenyeji wa mtaa huo ulio na idadi ya watu kiasi cha haja ambapo kuwasili kwao kulisababisha mhemko miongoni mwa wafuasi wao, walioonekana kusisimka kupita kiasi. Hali hiyo haikuwavutia macho walinda usalama, ambao walijaribu kuusambaratisha umati huo uliokuwa ukizidi kuongezeka kwenye kitongoji hicho. Haikueleweka ni sababu gani iliyowapa mshawasha askari hao kuwarushia wananchi vitoza machozi pamoja na kuwakung’uta marungu baadhi yao.

Feedback