Serikali ya kaunti ya Nairobi yawasimamisha kazi wafanyakazi 5 kwa kusanya hongo
13, Apr 2016
Kufuatia ufichuzi wa makala ya Jicho Pevu ambayo tumekuwa tukiyapeperusha kila Jumapili serikali ya kaunti ya Nairobi imetangaza kuwasimamisha kazi kwa muda wafanyakazi watano walioonekana kwenye makala hayo wakikusanya hongo kutoka kwa wachuuzi. Makala ya kibubusa cha kanjo yanafichua ufisadi uliokithiri katika City Hall.