Wateja wa benki ya Chase waendelea kukadiria hasara ikiwa tangu iwekwe chini ya mrasimu
12th April, 2016
Wateja wa benki ya Chase wanaendelea kukadiria hasara ikiwa siku ya sita sasa tangu iwekwe chini ya mrasimu. Charles Maina mmiliki wa kinyozi na mwajiri wa wafanyakazi kumi, sasa amelazimika kutafuta mbinu mpya, kwani hela zake zote zimo kwenye benki ya chase.