Haki dhaifu Sehemu ya kwanza - Jitimai ya Shule ya Upili ya Kyunguli
26th March, 2016
Miaka 15 iliyopita siku hii ya leo, wanafunzi 67 walifariki baada ya kuteketea katika bweni la shule ya upili ya kyanguli kaunti ya Machakos walipokuwa wamelala. Bweni hilo lilikuwa na uwezo wa kustahimili wanafunzi 60 lakini lilikuwa na wanafunzi 134 usiku huo. 58 waliteketea kiasi cha kutofahamika huku 9 wakifariki walipokuwa wakipokea matibabu. Mahakama kuu ilitoa agizo kwa serikali kuwalipa wazazi 63 waliofiwa shilingi milioni 40.95 3/3/2016 lakini malipo huenda yakawa ngoma. Sasa Mashirima Kapombe anaarifu kuhusu safari ya miaka 15 ya kutafuta haki kwenye makala maalum, haki dhaifu.