KTN Leo Wikendi Kamilifu Michezo - Harambee Stars yacharazwa Guinea Bissau
25th March, 2016
Rais wa shirikisho la kandanda nchini Nick Mwenda ameutetea uamuzi wa mkufunzi wa harambee stars Stanley Okumbi kuhusiana na uteuzi wa wachezaji waliocheza dhidi ya Guinea Bissau siku ya jumatano. Okumbi alilaumiwa kwa kuchezesha baadhi ya wachezaji wasio na uzoefu jambo lilofanya walazwe na guinea Bissau na kupunguza matumaini ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa barani afrika mwaka 2017. Suala hilo lilizua tumbojoto huku mashabiki wakionesha ghadhabu yao katika mitandao ya kijamii.