Waziri Joseph Nkaissery ametoa makataa kwa wezi wa mifugo kurudisha mifugo walioibiwa
10th February, 2016
Waziri wa ndani Joseph Nkaissery ametoa makataa ya wiki moja kwa wezi wa mifugo warudishe mifugo wote walioibiwa. Pia amewataka viongozi kuita mikutano ya kuhubiri amani. Nkaissery alikuwa anazungumza baada ya kuongoza mkutano wa siku mbili na viongozi wa kaunti ya Samburu na mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusuusalama Asman Kamama.