x News The Standard Digital KTN Prime KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS Tutorsoma Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
x
x

Mshukiwa wa uraibu wa mihadarati akupatikana amefariki mjini Mombasa

24, Jan 2016

Kutekelezwa kwa vita dhidi ya mihadarati mjini Mombasa kumetiliwa shaka na baadhi ya wenyeji baada ya mshukiwa wa uraibu wa mihadarati kupatikana amefariki. Mwili wa jamaa huyo ambaye alikuwa kijana wa kurandaranda mtaani ulipatikana uwanja wa makadara mjini humo. Waliomfahamu wanasema marehemu alitoka jela karibuni na alikuwa na nia ya kujiunga na kituo cha kumrekebisha aachane na mihadarati lakini hakuwa na pesa, hali iliyomlazimu kurejelea uraibu huo. Familia hizo za kurandaranda zinadai wenzao hufariki kila kukicha kutokana na mihadarati lakini masaibu yao hayatiliwi maanani. Sasa wanamtaka rais uhuru kenyatta na gavana ali hassan joho kutimiza ahadi zao kupiga vita mihadarati haswa kwa kuwapa nafasi ya kujirekebisha waraibu wa mihadarati.

RELATED VIDEOS


Feedback