Zahanati wapotibiwa Mzee Jomo Kenyatta na wenzake wanne wa Kapenguria 6 Turkana
19th December, 2015
Hospitali ya rufaa ya kaunti ya Turkana mjini Lodwar ina chumba cha kutamanika. Ni chumba kilicho na historia ya Kenya. Chumba hicho ndicho kilichokuwa zahanati alipotibiwa baba wa taifa Mzee Jomo Kenyatta na wenzake wanne kati ya wale wa Kapenguria 6 walipokuwa wamefungwa mjini Lodwar.