Mshambuliaji wa Gor Mahia Micheal Olunga ateuliwa mchezaji bora wa kandanda mwaka 2015
11, Dec 2015
Mshambuliaji wa Gor Mahia Micheal Olunga ameteuliwa mchezaji bora wa kandanda mwaka 2015 katika tuzo za FOYA. Wachezaji wengine waliotuzwa ni Boniface Oluoch aliyeshinda tuzo ya mlinda lango bora, Karim Nzigiyimana akatawazwa mlinzi bora naye Frank Nuttal akachukua taji la mkufunzi bora. Erick Johana wa Mathare alitawazwa kiungo wa kati bora.