Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi atekwa nyara Kisumu
3rd December, 2015
Familia moja huko Kisumu inamtafuta mwana wao aliye na umri wa miaka ishirini ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi tawi la Kisumu anayeaminika kutekwa nyara Ijumaa wiki jana akitoka chuoni kuelekea nyumbani. Kwa mujibu wa kamanda wa kaunti ya Kisumu Nelson Njiiri mshukiwa mmoja ametiwa nguvuni kuhusiana na tukio hilo.