Raila Odinga: "Uchumi wa taifa la Kenya unazama huku madeni yakizidi"
21st October, 2015
"Uchumi wa taifa la Kenya unazama huku madeni yakizidi " ni kauli ya aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa muungano wa CORD Raila Odinga aliyerejea kutoka taifa la korea kusini mapema hii leo , kiongozi huyo wa upinzani amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuwajibika katika kuboresha uchumi wa Kenya, Hussein Mohammed alihudhuria mkutano huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.