Marufuku ya kutoka nje yaanza rasmi mjini Garissa
4th April, 2015
Kufuatia ongezeko la visa vya kigaidi humu nchini , serikali imetoa majina ya baadhi ya wahusika wakuu wa mashambulizi hayo ya kigaidi. Ni hapo jana tu jina la mhusika mkuu wa shambulizi la Garissa Mohamed Mohamud lilichapishwa huku serikali ikiahidi kutoa zawadi ya shilingi Milioni Ishirini pesa taslimu kwa yeyote atakayetoa taarifa itakayopelekea kukamatwa kwake.