Makamishna walioteuliwa na rais Uhuru kutafuta suluhu ya mzozo Makueni wahojiwa na kamati ya seneti
24th February, 2015
Kamati ya seneti kuhusu serikali za ugatuzi mapema hii leo iliwahoji makamishna walioteuliwa na rais Uhuru Kenyatta ili kutafuta suluhu ya mzozo unaoikumba kaunti ya Makueni
Rais Kenyatta alipendekeza makamishna sita ambao wataongozwa na mwenyekiti wake Mohammed Nyaoga. Wengine watakaohusika katika shughuli hiyo ni mwenyekiti wa tume ya huduma kwa polisi Johnston Kavuludi , Emily Gatuguta , Profesa Harrison Mathioya , Alice Wairimu na wakili Taib Ali Taib. Kuhojiwa kwao kuliendelea kwa takriban saa sita huku kila mmoja wao akipata muda wa kuhojiwa. Mwezi wa Novemba mwaka jana , zaidi ya watu 3000 kutoka kaunti ya Makueni walikita kambi katika jumba la Harambee na kumkabidhi rais Kenyatta malalamishi yao kuhusiana na uongozi wa kaunti hiyo. Kamati hiyo inatarajiwa kutoa pendekezo lake hapo kesho.