×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Rais Mstaafu Daniel arap Moi ataka serekali kuongeza idadi ya walimu nchini

21st February, 2015

Rais wa pili wa jamhuri ya kenya daniel arap moi ameitaka serikali kuongeza idadi ya walimu katika shule humu nchini ili kuhakikisha kuwa kila darasa lina wanafunzi 40 kama njia mwafaka ya kushughulikia kila mwanafunzi vilivyo. Akizungumza mapema hi leo katika shule ya msingi ya moi kabarak kwenye sherehe ya kuwatuza waliofanya vyema mwaka jana, moi amedokeza kuwa ubora wa elimu unaathirika kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi darasani. Moi amedokeza kuwa nchi na jamii kwa jumla ina uwezo wa kutoa mwelekeo mwafaka hususan kwenye masuala ya elimu kwa watoto akidai kuwa shule za msingi ndizo zenye jukumu la kutoa nguzo ya maisha ya baadaye. Hata hivyo moi ameuchesha umati uliohudhuria sherehe hiyo pale alipouimba wimbo mmoja alioutumia kama mfano wa jinsi jamii inavyoweza kujikakamua na kujitegemea katika kuboresha maisha.
.
RELATED VIDEOS