Mvulana wa miaka 15 ajeruhiwa na lori lililowagonga mifugo 55 katika barabara ya Mai Mahiu-Naivasha
30, Jan 2015
Mvulana wa miaka 15 ambaye ni mchungaji mifugo katika eneo la naivasha amejeruhiwa na trella lililowagonga mifugo 55 katika barabara kuu ya mai mahiu- naivasha. Mvulana huyo alijeruhiwa alipojaribu kuwaondoa baadhi ya kondoo aliokuwa akiwaongoza wavuke barabara wakati trella hilo lilifika na kuwaponda ponda na kufululiza safarini.