Bandari ya Mombasa yadaiwa haiwafaidi wenyeji
15, May 2014
Wanachama wa baraza la kaunti ya Mombasa wamelalama kwamba licha ya bandari ya Mombasa kuwa katika kaunti hiyo , wenyeji hawajawahi faidika kwa vyovyote vile . Wanachama hao sasa wanataka bandari hiyo kuwa chini ya mamlaka ya serikali ya kaunti ya Mombasa. Akihutubia wanahabari , mwakilishi wa wadi ya tononoka saad faraj amesema kuwa haki za wakaazi wa Mombasa kufaidika kutokana na bandari hiyo zimehifadhiwa katika sehemu ya nne ya katiba.