Mauaji ya Abubakar Sharrif maarufu kama Makaburi yameshutumiwa vikali na viongozi wa kidini
2nd April, 2014
Mauaji ya Abubakar Sharrif maarufu kama Makaburi yameshutumiwa vikali na viongozi wa kidini, mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na vyombo vya usalama na kuyataja kuwa mauaji ya kiholela yanayochochea chuki na uhalifu zaidi mjini Mombasa. Vyombo vya usalama vimesema uchunguzi tayari umeanzishwa kubaini waliotekeleza mauaji hayo.