Ziara ya rais Uhuru Kenyatta Kuwait
19th November, 2013
Rais Uhuru Kenyatta ameyashawishi mataifa ya Uarabuni kuwekeza kwa wingi barani Afrika ili kukuza na kudhibiti uhusiano wao. Akizungumza huko Kuwait baada ya kuhudhuria kongamano la tatu la mataifa ya Afrika na Uarabuni, rais Kenyatta mataifa ya Afrika na wenzao wa Uarabuni wana historia ya muda mrefu na kwamba malengo yao hayajaachana pakubwa. Aliongeza kwamba waasisi wa urafiki na uhusiano wa mataifa ya kiarabu na Afrika walikuwa na lengo la kukuza maendeleo na ufanisi ambao kila upande unauzingatia. Na kuweka gundi zaidi katika urafiki huu, mataifa haya hayana budi ila kushirikiana kibiashara, na masuala mengine ambayo yanaathiri mataifa ya kiafrika na ya kiarabu. Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana Kuwait, mbali na mikataba na miradi ya uchumi, pia utajadili masuala ya ugaidi, biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya na uharamia, pamoja na usalama wa maeneo ya Afrika yanayopakana na mataifa ya kiarabu. Viongozi 65 kutoka Afrika, Uarabuni na mataifa ya Asia wanahudhuria mk