Wahome Mutahi "Whispers" akumbukwa
20th July, 2013
Ni miaka kumi sasa tangu kenya kumpoteza, wahome mutahi kwa jina maarufu, whispers, ambaye uandishi wake uliwaacha wengi wakivunjika mbavu kwa usheshi. Kwa utani wake aliwapa hata majina ya utani familia yake, wanawe ilikuwa ni pajero, investmenty na junior. Mkewe alikuwa ni Thatcher. Whispers alikufa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutoa uvimbe shingoni na hadi leo familia yake inamlaumu daktari mhusika. Ktn ilipata fursa ya kuzungumza na mamake Octavia Muthoni, nyumbani kwake huko tetu, kaunti ya nyeri.