Naibu Rais William Ruto akutana na viongozi wa dini katika hoteli moja jijini Nairobi

KTN Leo | Thursday 12 Jul 2018 7:52 pm

Naibu rais William Ruto akutana na viongozi wa dini katika hoteli moja hapa jijini Nairobi. mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa kanisa katoliki akiwemo kadinali john njue ulipangwa na baadhi ya wabunge kwa lengo la kuleta utangamano wa kitaifa. Haya yanajiri siku tano tu baada ya naibu rais kutangaza kuwa hakuna jamii yoyote iliyo na deni lake la kisiasa.