Kidero amulikwa upya kuhusiana na kampuni ya sukari ya Mumias

KTN Leo | Thursday 12 Jul 2018 7:32 pm

Viongozi kutoka eneo la magharibi ya Kenya sasa wanamtaka kiongozi wa mashitaka ya umma  na mkurugenzi wa idara ya upelelezi kumkamata na kuanzisha mashtaka dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Evans Kidero kwa kile wanachodai alifuja mabilioni ya fedha katika kampuni ya sukari ya Mumias. Kulingana na viongozi hao, Kidero aliangusha kampuni ya Mumias Sugar na kuwaacha wakulima wa miwa wakiwa maskini alipokuwa mkurugenzi mkuu katika kampuni hiyo.