Mkasa wa bwawa la Solai: Jopo la kuwasaidia waathiriwa labuniwa

KTN Mbiu | Wednesday 13 Jun 2018 5:11 pm

Jopo litakalojumuisha mashirika mbali mbali limebuniwa kuwasaidia waathiriwa wa mkasa wa kuporomoka kwa bwawa la Patel katika eneo la Solai kaunti ya Nakuru kurejelea maisha yao ya kawaida.  Bwawa hilo lilivunja kingo zake mwezi mmoja uliopita na kusababisha vifo vya watu 47 na kuacha uharibifu mkubwa wa mali kundi la maafisa kutoka serikali ya kaunti likiongozwa na gavana Lee Kinyanjui na kamishna wa jimbo hilo Mongo Chimwanga limewaambia waathiriwa wa mkasa huo kwamba  wote watapigwa msasa ili kukadiria wanaohitaji msaada