Watu wanane wafariki kwenye ajali ya Kyumbi iliyohusisha matatu na lori

KTN Mbiu | Sunday 22 Apr 2018 4:44 pm

Watu wanane wamefariki kufuatia ajali ya barabarani katika eneo la Kyumbi kwenye barabara kuu ya Nairobi   Mombasa.Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa nane alfajiri ya leo wakati matatu iliyokuwa ikisafiri kutoka eneo la loitoktok iligonga lori lililokuwa limeegeshwa. Abiria wengine wanne wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa 
hospitalini kwa matibabu.