Jamii ya Sikh yatoa mchango wa kujenga tawi la huduma za kujifungua katika hospitali ya Kericho

Leo Mashinani | Tuesday 17 Apr 2018 12:58 pm

Jamii ya Sikh huko kericho imechanga shilingi milioni 10 kwa ujenzi wa tawi la huduma za kujifungua katika hospitali ya Kericho. Chumba kikubwa zaidi cha jamii ya Sikh ni kile kilichoko katika kaunti ya Kericho. Lengo kuu la ujenzi wa tawi la kujifungua katika hospitali hiyo ni kuwasaidia kina mama kujifungua na kupata huduma kwa karibu na haraka.