WafugajiKajiado wapata teknolojia inayowaruhusu kutumia simu kutafuta malisho ya mifugo

Leo Mashinani | Tuesday 17 Apr 2018 12:54 pm

Teknolojia  mpya imeletwa kwa wafugaji kaunti ya Kajiado inayowaruhusu kutumia simu zao kung'amua ni wapi yalipo malisho ya mifugo wao.  Teknolojia hiyo imeletwa na shirika linalojiita BSI chini ya usimamizi wa mratibu wa mradi huo Wadela Ngachi.  Ni hatua inayolenga kuwawewezesha kujua mara moja kupitia mtandao kwenye rukono zao, kuwa malisho yako wapi.