Watu walio na matatizo ya figo sasa wanatoa wito kwa serikali

KTN Leo | Tuesday 13 Mar 2018 7:56 pm

Watu walio na matatizo ya figo sasa wanatoa wito kwa serikali kuwahusisha katika mpango wa hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu nchini NHIF ili kuwarahisishia mzigo wa matibabu. Waathiriwa wa ugonjwa huo aidha wanaitaka serikali kupunguza gharama ya dawa wanazonunua baada ya kupitia hali hiyo.