Mtu mmoja auawa na polisi wanne kujeruhiwa baada ya Al shabaab kuwashambulia Lamu

KTN Leo | Saturday 13 Jan 2018 7:39 pm

Mtu  mmoja amefariki huku maafisa wa polisi wanne wakijeruhi

        baada ya wapiganaji wa alshabaab kushambulia msafara wa

        mabasi uliokuwa ukielekea malindi na mombasa majira ya saa

        tano hii leo. Kwa mujibu wa taarifa ya serikali kulikuwa

        na  makabiliano makali kati ya vikosi vya usalama vilivyokuwa

        vikisindikiza mabasi hayo na wapiganaji hao. Wapiganaji hao

        waliteketeza moto baadhi ya magari ya maafisa wa usalama.

         seneta wa lamu anwar olei?tiptip amezungumzia kisa hicho

        na kuvitaka vikosi vya usalama kuwa macho zaidi