Tusker kutwaa ushindi dhidi ya viongozi wa sasa wa ligi Gor Mahia katika KPL

Sports | Friday 21 Apr 2017 7:40 pm

Michuano ya ligi kuu nchini yanatajiwa kuwa na msisimuko mkubwa huku mabingwa watetezi Tusker wkiwa na kibarua cha kujaribu kutwaa ushindi dhidi ya viongozi wa sasa wa ligi Gor Mahia kwenye mechi itakayoandaliwa kwenye uwanja wa afuraha siku ya jumamosi. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na msisimuko mkubwa huku timu zote zikiwa na ari ya kuonyesha ubabe wao. Kutakuwa na mechi tofauti huku Posta Rangers nao wakiwa na kibarua dhidi ya Kariobangi Sharks. Katika michuano tofauti, Sofapaka ambao wanashikilia nafasio ya nne kwenye jedwali watawakaribisha Kakamega Homeboyz katika uwanja wa Camp Toyoyo nao wana zoo Kericho ambao wanashikilia nafasi ya mwisho kwenye jedwali wakiwa na kibarua ugenini bungoma dhidi ya mibabe wa Nzoia Sugar. Thika United watakuwa wenyeji wa Afc Leopards na Ulinzi Stars igaragazana na Mathare united.