.
12th May, 2021
Wakazi wa kaunti ya Nakuru watasubiri zaidi kabla ya kupata maji kutoka kwa bwawa la Itare. Hii ni ni baada ya kubainika kuwa serikali bado haijapata mwanakandarasi mpya wa kuendelea na mradi huo uliokwama miaka mitatu iliyopita. Katika taarifa kwa wanahabari, afisa wa kampuni ya Central Rift Water Works Development Agency Joseph Salee na kamishna wa kaunti ya Nakuru Erastus Mbui walishindwa kuelezea iwapo mradi huo umezingatiwa katika bajeti ya mwaka 2021/22, ambayo ndiyo wa mwisho chini ya Utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.