×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Uvuvi Haramu Pwani: Nahodha wa mashua ya kuvua samaki aina ya kamba akamatwa Tana River

14th April, 2021

maafisa wa huduma kwa wanyama pori wamemkamata nahodha wa mashua moja ya kuvua samaki aina ya kamba katika eneo la kipini kaunti ndogo ya tanadelta huko tanariver ambayo inadaiwa ilikuwa ikifanya uvuvi haramu bahari hindi.maafisa hao pamoja na maafisa wa serikali ya kaunti ya tanariver walifanikiwa kumkamata salim kolombo tawfiq afisa mkuu wa chombo cha uvuvi cha mv roberto, mali ya tajiri mmoja mwenye asili ya kiitalia. ripoti za polisi zinaonyesha kwamba mashua hiyo ilikuwa ikitumia vifaa vya uvuvi vilivyopigwa marufuku haswaa kifaa muhimu cha kumzuia na kumrejesha kasa majini wakati wa uvuvi. katika ushahidi ulioonyeshwa kwa wanahabari kulikuwa na aina moja ya samaki aina ya guiter ambaye amepigwa marufuku na papa wadogo walio vuliwa kinyume na sheria ya usimamizi na maendeleo ya uvuvi (35 ya 2016).

.
RELATED VIDEOS